Tuesday, August 30, 2011

MASIKINI KANUMBA NA AUNT DAH WATIA HURUMA


Mastaa wa filamu Bongo, Steven Kanumba na Aunt Ezekiel ‘Gwantwa’ wamepatwa na aibu baada ya magari yao kupata hitilafu wakiwa kwenye safari tofauti.

Aunt, alizimikiwa na gari lake eneo la Bamaga, Mwenge, wakati la Kanumba tairi lilikita kwenye mchanga na baadaye kuzimika kwenye eneo la Nunge, Kigamboni (pichani).

Paparazi wa blog BUGU THE GREAT aliyanasa matukio hayo kwa nyakati tofauti amebaini kuwa Aunt alikwenda kumtembelea shosti wake Bamaga lakini aliporudi kwenye gari halikuwaka.

Kutokana na sekeseke hilo, ilibidi rafiki wa Aunt, muigizaji Nice Chande afungue ‘boneti’ akitapatapa kuliwasha bila mafanikio.

Hata hivyo, baada ya kama dakika 10 za kutapatapa, gari lilikubali ‘stata’ likawaka na safari ikaendelea.
Aunt alipoulizwa na mwandishi wetu kuhusu gari lake kukata moto alijibu: “Niliacha redio inawaka, sasa betri ilipungua chaji ndiyo maana ilisumbua kuwaka.”

Kwa upande wa Kanumba, alikuwa anakwenda kutoa msaada kwenye kituo cha kulea watoto mayatima lakini lilipata pancha tairi la mbele.

Hata hivyo, dereva wa Kanumba, Seth Bosco alimtoa wasiwasi staa huyo kuwa kuna tairi la kubadilisha (spea tairi).

Habari zinasema kuwa baada ya tairi kubadilishwa, gari lilikita kwenye mchanga na likazima kwa dakika kadhaa.

Baadaye, walitokea waungwana ambao walimsaidia Kanumba na dereva wake kulisukuma gari hilo mpaka kwenye eneo ambalo halina mchanga.

BLOG HII  imeelezwa kuwa gari hilo lilipoondolewa mchangani, liliweza kuwaka hivyo Kanumba kuendelea na ratiba zake

Friday, August 26, 2011

NANI ANA KUBWA ZAIDI YA WENZAKE?

IMEBAINIKA kuwa, baadhi ya mastaa Bongo wameingia katika zoezi la kushindana kukuza makalio huku kila mmoja akitumia njia anayoijua.

Uchunguzi wa Blog hii umegundua kuwa, mastaa wanaofanya hivyo wengi ni wasanii wa filamu ambao wanaamini wakiwa na maumbile makubwa soko lao katika tasnia hiyo nalo linakuwa juu.

Wakizungumza na mwandishi wetu wa BLOG BUGU THE GREAT kwa nyakati tofauti baadhi ya wasanii walioomba majina yao kutoandikwa gazetini walidai kuwa, ni ukweli usiofichika kuna wenzao wanadiriki kutumia dawa za kichina ili kukuza makalio.

“Yaani iko wazi kwamba, wenye makalio makubwa kwanza wanapendwa na wanaume wengi lakini pia kwenye filamu wale wanaojua kuuvaa uhusika vizuri dau lao huwa kubwa. Muangalie Skaina, umbile lake linalipa na ndiyo maana anakula shavu kwenye video za muziki na filamu kibao.

“Mwangalie Efrancia, katoka maisha Plus alipoingia kwenye filamu tu, amekula shavu la kutosha kwa sababu ya umbile lake.

“Sasa wengine wanataka kuwa hivyo, wenzao makalio yao ni orijino ila kuna ambao wanatumia dawa kuyakuza na wengine wanakula sana ili wanenepeane,” alidai mmoja wa wasanii hao mwenye jina kubwa Bongo.

Aidha, juzikati hii ilinasa picha inayowaonesha wasanii Jennifer Mwaipaja ‘Shumileta’ Zamda Salim na Skaina Ally (Pichani juu)wakionesha makalio yao huku baadhi ya wadau wakihoji kama ni ya kichina au ya orijino.

Walipotafutwa na kuulizwa kama walikuwa wakishindana kuonesha mwenye makalio makubwa na kama yao ni ya kichina, mastaa hao walisema kuwa yao ni ya asili na hawakuwa wakishindana bali lilikuwa ni pozi tu.SASA EBU TULEZANE NANI ANA KALIO LA KICHINA?

Wednesday, August 24, 2011

MAMBO YA FACEBOOK:LULU NA REHEMA WAMGOMBANIA JUSTINE BEIBER KWENYE FACEBOOK LULU ASEMA YUKO TEYARI KUTEMBEA UCHI


NI kituko cha mwaka kwa mastaa wawili Bongo, muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Mshiriki wa Miss Kiswahili 2009, Rehema Fabian ‘Video Queen’ kumgombea mwanaume ambaye hana habari nao, blog hii kwa kupitia kwa mwana haraki wetu MUGU THE GREAT

Lulu (18) ndiye alikuwa wa kwanza kuelezea hisia zake kupitia blog moja ivi ambalo tumbo moja na blog hii, hivi karibuni ambapo alikaririwa akisema kuwa, anampenda msanii kinda wa Marekani, Justin Bieber (19) na kwamba siku jamaa huyo akitia maguu Bongo, yuko tayari kutembea uchi kutoka kwao hadi sehemu atakapokuwa msanii huyo.

Akizungumza na mwandishi wa blog hii jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, Rehema alisema alisikitishwa sana na habari hiyo hivyo alimpigia simu Lulu na kumpa za uso kuwa aache mara moja kumpenda Bieber kwani yeye ndiye alikuwa wa kwanza kumpenda msanii huyo.
“Kiukweli kutoka moyoni mwangu nampenda sana Bieber ndiyo maana niliamua kuchora ‘tatuu’ ya jina lake mkononi mwangu,” alisema Rehema na kuongeza:

“Hiyo yote ni kwa sababu nampenda Bieber kupita maelezo na nilimweleza Lulu juu ya hilo, lakini cha ajabu naye amekwenda kujichora na kuniwahi kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa anampenda msanii huyo.

“Namuomba Lulu aniachie Bieber wangu. Siku nikikutana na mwanamuziki huyo, hakutakuwa na maswali zaidi ya kujikabidhisha kwake hata kama hanitaki.”

Hivi karibuni Lulu aliweka wazi hisia zake juu ya kinda huyo kutoka katika ardhi ya Rais Obama, Marekani huku akitafuna maneno kuwa huwa anajisikia maradhi ya moyo amuonapo Bieber na mpenzi wake Selena Gomez. 


hata ivyo Lulu amejibu mapigo hayo na kusema Rehema hana jipya kwasababu teyari anamawasiliano na star huyo wa pande za Obama na asishangae siku atakayoona amekwea pipa kuelekea pande hizo za Obama kumfuata sweet wake huyo ambaye anampenda kupita kula,lulu amabaye amechora Tatoo ya Beiber mgongoni kwake amesema yu teyari tembea mtupu toka kwako TABATA anakoishi mpaka pale atakapofikia Beiber siku akitika maguu ndani ya Jakaya Land

Tuesday, August 2, 2011

KWA BABU LOLIONDO SASA HAKUNA DILI MAMBO YOTE SASA NI KWA MTOTO HUKO MALEMA

Mtoto Subira Ally (12), Mkazi wa Kijiji cha Malema, Kata ya Maratani, wilayani Nanyumbu, mkoani Mtwara ameonekana kumpindua Babu wa Loliondo, Mchungaji Ambilikile Masapile (pichani) kwa kupata wateja wengi ambao wanakwenda kutibiwa.

Kupinduliwa kwa Babu kumetafsiriwa na watu baada ya kuonekana sasa nyumbani kwake Kijiji cha Samunge hakipati wageni wengi kama ilivyo Kijiji cha Malema anakokaa Subira ambako  wageni kutoka mikoa mbalimbali na nchi jirani hufurika kila kukicha.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, mtoto Subira alisema kuwa siku moja ,  Aprili mwaka huu akiwa amelala alioteshwa ndoto iliyokuwa ikimuelekeza kuwa anatakiwa atoe tiba kwa njia ya kikombe kwa kutumia mzizi wa mti uitwao Mkong’oto unaopatikana hapo nyumbani kwao, hivyo kumjulisha mama yake mkubwa anayeishi naye.

“Niliambiwa kuwa dawa hiyo itakuwa inatibu Ukimwi, kisukari, kuponya vipofu, viziwi, na wote ambao miili yao itakuwa imekufa ganzi au kupooza,” alisema Subira.

Aliongeza kuwa dawa hiyo ya kikombe alioteshwa kuwa iwe ikinunuliwa kwa gharama ya shilingi 500. Alipoulizwa ni watu wangapi ambao amewatibu tangu alipoanza kazi hiyo alisema ni wengi sana.

“Wagonjwa ni wengi sana ambao wamepata kikombe na wanaendelea kufika hapa nyumbani,” alisema huku akiwa na mama yake mkubwa aliyefahamika kwa jina moja la Binti Ismail.Subira alisema licha ya kutibu wananchi wa Tanzania, amekuwa akipokea wageni wengine kutoka nje ya nchi kama vile Msumbiji na Malawi.

Aliongeza kuwa licha ya wagonjwa wengi kutoka Tanzania bara, amepokea wengine kutoka  Visiwani Zanzibar na anakumbuka mmoja alikuwa na matatizo ya miguu ambayo ilikuwa imekufa  ganzi kwa miaka mitano. “Sasa mgonjwa huyo wa Zanzibar ganzi imekwisha na anatembea vizuri, amemshukuru sana Mungu.” Mama mkubwa wa binti huyo, aliyefahamika kwa jina la Binti Ismaili alithibitisha mwanaye kuoteshwa na kutoa tiba hiyo.

MASHUHUDA

Naye mama mmoja  aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Sharifa  mkazi wa Tandika Mikoroshini  jijini Dar es Salaam aliyezungumza na mwandishi wetu hivi karibuni alisema kuwa, alikuwa muathirika wa ugonjwa wa Ukimwi lakini baada ya kutumia dawa ya mtoto huyo na kwenda kupima ameonekana hana virusi vya maradhi hayo.

“Baada ya kutumia dawa ya Mkong’oto nimepona,nilikwenda kupima katika Hospitali ya Maratani mkoani Mtwara  na kuthibitishiwa na daktari aliyenipima aitwae Dk.Namihambi  kuwa sina virusi. Nangoja kupima mara ya pili kwa uhakika zaidi,” alisema.

Aidha, baba mmoja ambaye aliomba jina lake kuhifadhiwa alisema kuwa alikuwa na ugonjwa wa Ukimwi lakini sasa hana baada ya kupimwa katika Hospitali ya Mkomaindo, Masasi.

WAZIRI WA AFYA ALICHOSEMA

Mara baada ya Babu Masapile kutangaza kuoteshwa kutoa tiba ya magonjwa sugu, watu wengi wameibuka kutoa tiba hiyo na wananchi kufurika kupata kikombe.

Hata hivyo, wiki iliyopita gazeti hili lilimkariri Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda akisema kuwa katika tafiti za kitaalamu dawa za mitishamba hazijathibitishwa kutibu Ukimwi.

Kauli hiyo ilitolewa na waziri huyo wakati anazindua Kituo cha Matibabu ya Wagonjwa wa Ukimwi na Mafunzo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Dk. Mponda alisema wagonjwa wa Ukimwi wanatakiwa kutumia dawa za kurefusha maisha (ARV) na akawataka waende kwenye vituo vya afya kupewa.“Wagonjwa wanaokwenda kupata tiba asili waache kwa kuwa bado zinafanyiwa utafiti,” alisisitiza Waziri Mponda.