JACKLINE WOLPER ABANWA
Hemed Kisanda na Jelard LucasMastaa ‘kapo’, Jacqueline Wolper na Nassib Abdul ‘Diamond’ ambao uhusiano wao kimapenzi umekuwa ukitengeneza vichwa vya habari, wanaendelea kujikanganya, ishu kamili ipo aya zinazofuata.The First Class Paper, Ijumaa lilimnasa Jacqueline Jumatatu ya wiki hii, saa 4 usiku na kumbana kwa maswali mfululizo kuhusu Diamond kutokana na ukweli kwamba, yeye ndiye yupo mstari wa mbele kukanusha ukweli.Akiwa amekolea ‘make up’ tayari kurekodi muvi mpya inayoitwa Mafisadi, Kijitonyama Sayansi, Dar, Jacqueline alisema kwa kujikanyaga kwamba anamfahamu Diamond kama msanii mwenzake na wanashirikiana tu kikazi.“Namfahamu kama mwanamuziki na sijawahi kumjua kwa jambo lingine zaidi,” alisema Jacqueline.Alipouliza ushirikiano gani walionao, yeye akiwa staa wa filamu na Diamond ni mwanamuziki, staa huyo ambaye pia anatambulika kama pacha wa Ijumaa Sexiest Girl 2008-09, Irene Uwoya, alijibu:“Diamond ana filamu yake anayotaka kuitoa na amesema atashirikiana na mimi. Amesema mimi nafaa kushiriki muvi yake, kwahiyo tunashirikiana kwa staili hiyo.”Hata hivyo, akionesha kuwa amejipanga kukwepa kila swali, Jacqueline alitoa macho kwa mshangao, pale paparazi wetu alipomueleza kwamba zipo ‘data’ zinazomthibitisha alipomkoromea Diamond kwa kuvujisha siri ya uhusiano wao.Jacqueline akiwa haamini alichokisikia, alisema: “Mmh, nanyi mnafuatilia vitu!”Mrembo huyo alikosa swali alipotajiwa jina la hoteli moja iliyopo Magomeni Kagera, Dar ambayo ndiyo hukutana na Diamond kwa ajili ya mambo yao.Kijasho kilimtoka Jacqueline, alipoambiwa kuwa alimpigia simu Diamond na kumlaumu kwamba hana siri, siku ambayo uhusiano wao wa kimapenzi ulipoandikwa kwa mara ya kwanza na gazeti la Risasi.Badala ya kupangua hoja, Jacqueline alisema: “Nyinyi watu wa Global Publishers (wachapishaji wa Ijumaa) ni hatari sana, yaani hata hilo mnajua?”Alipozungumza hivyo, Jacqueline alinyanyuka na kuondoka kwa maelezo kwamba muongozaji wake alikuwa akimhitaji kwa ajili kwa ajili ya kuanza kurekodi filamu.Baada ya kuachana naye, siku iliyofuata, paparazi wetu ‘alimbananisha’ tena Jacqueline Bamaga Mwenge, Dar na kuendeleza maswali juu ya uhusiano wake na Diamond ambapo alijibu:“Ndani ya nafsi yangu najua Diamond ananipenda sana lakini mimi siwezi kutoa penzi langu kwake kwa sababu naogopa umri wake mdogo atadata.”Pamoja na majibu hayo, Ijumaa lina vielelezo kuwa Jacqueline na Diamond wanaitana majina ya sweet na honey lakini wao wenyewe hawataki watu wajue.endelea kusoma blog yangu ili kujua nini kitaendelea
No comments:
Post a Comment