Friday, July 1, 2011

MAKUBWA YAIBUKA KWA BABU LOLIONDO

SIRI NZITO KUHUSU VIGOGO WANAODAIWA KUTIMKIA KWA BABU,MCHUNGAJI AMBILIKILE MWASAPILE IMEFICHUKA,HUKU MAAJABU YA KIKOMBE CHAKE CHA KUGAWIA DAWA,YAKIBAKI NA VIULIZO VINGI.
KWA SASA, MCHUNGAJI AMBILIKILE A.K.A BABU AMBI WA LOLIONDO,AMESHIKA UBONGO WA WENGI HUKU IKIDAIWA KWAMBA,VIGOGO KIBAO WAMEPATA TIBA YAKE LAKINI HAWATANGAZI.
THE BLOG www.ibrahimthetycoon.blogspot.com LIMEBAINI YAFUATAYO; MAAJABU YA BABU AMBI YALIANZA ZAMANI LAKINI VIGOGO WALIZUIA MATANGAZO YASIFIKE KWA WENGI ILI WATIBIWE WENYEWE KWANZA.
KWA BABU AMBI NI NOMA, KWANI HAKUNA U-VIP WALA UKIGOGO,VIONGOZI NA VYEO VYAO WAMEPANGISHWA FOLENI. KIKOMBE CHA DAWA NI CHA MAAJABU,KWANI ILI TIBA IFANYE KAZI NI LAZIMA MTU ANYWE ANAONEKANA,VINGINEVYO ATAAMBULIA PATUPU.
UWEZO ULIOMO NDANI YA MACHO YA BABU AMBI NI ISHU NYINGINE,KWANI WALIOPEWA TIBA YA UKIMWI AMBAO WALIUPATA KWA UZINZI,ALIWABAINI HARAKA NA KUWAAMBIA WASIRUDIE.
KIKUNDI KIDOGO KINACHOKADIRIWA KUWA NA WATU 10,KINADAI KUONA MIUJIZA YA BABU AMBI, KWA HIYO KINATEMBEA KWENYE HOSPITALI MBALIMBALI NA KUTAKA WAGONJWA WASIPOTEZE MUDA,BALI WAENDE LOLIONDO.
WATU WANAOUNDA KIKUNDI HICHO,WANADAI WAO WALIKUWA WAATHIRIKA WA UKIMWI LAKINI WAMEPONA BAADA YA KUPATA DOZI KUTOKA KWA BABU AMBI.
KIONGOZI WA KIKUNDI HICHO,AFANIELI ZEFANIA ALIMWELEZA MWANDISHI WETU KUWA, ANASHANGAA MPAKA LEO KUNA WATU WANAJIULIZA KUHUSU UWEZO WA BABU AMBI.
“TUNATEMBEA MAHOSPITALINI NA KUWAELEZA WAGONJWA WA UKIMWI WASIPOTEZE MUDA WAO MTAANI,WAENDE KWA BABU LOLIONDO.YULE ANATIBU.MIMI NA WENZANGU TULIKUWA TUMEKATA TAMAA LAKINI LEO TUNASHUKURU TUMEPONA.
“UKIMWI UMETESA WENGI TENA KWA MUDA MREFU.AJABU NI KUWA HIVI SASA BABU ANATIBU KWA GHARAMA NAFUU TENA NDANI YA KIPINDI KIFUPI.UKINYWA DAWA LEO,BAADA YA WIKI UKIENDA KUPIMA UNAKUTWA NI MZIMA,” ALISEMA ZEFANIA.
SI WOTE WANAOENDA KWA BABU LOLIONDO WANAUMWA UKIMWI,KISUKARI,KIFUA NA MAGONJWA MENGINE SUGU,KWANI IMEBAINIKA KUWA,WENGINE WANAKWENDA HUKO KUSAKA NGUVU ZA KIUME.
GAZETI HILI LIMEPATA NYETI KWAMBA KUNA KIGOGO ALIYEKUWA NA HOFU YA NDOA YAKE KUVUNJIKA LAKINI BAADA YA KUPATA KINYWAJI KUTOKA KWA BABU,HIVI SASA MAMBO POA.
HABARI ZINASEMA KUWA, HIVI SASA KIGOGO HUYO ANAMUDU VYEMA KUMTULIZA MKEWE NYUMBANI KWA SABABU ‘JONGOO ANAUPANDA MTUNGI’ INAVYOTAKIWA.
“UZURI KIGOGO MWENYEWE NI MTU MWENYE SHUKRANI. ANATAFUTA JINSI YA KUMFIKISHIA ASANTE ZAKE BABU WA LOLIONDO LAKINI ANAHOFIA FOLENI NA JINSI YA KUMPA HIYO ASANTE,”ALISEMA DEREVA WA KIGOGO HUYO NA KUONGEZA:
“KINGINE ANAOGOPA KUONEKANA KWA WATU.YEYE ALIPATA TIBA MWANZONI KABISA,KWA HIYO SASA HIVI AKIRUDI ATAKUWA ANAJICHORESHA,ILA UKWELI NI KWAMBA JAMAA KWA SASA MAMBO POA NA HATA NYUMBA NDOGO KAJIWEKA.”
INAELEZWA KWAMBA, KIKOMBE CHA BABU NI CHA MIUJIZA KWA SABABU DAWA HIYO IKIHAMISHIWA KWENYE KIKOMBE KINGINE HAITIBU.
MTI UNAODAIWA KUTIBU NI GERESHA TU,KWANI BILA MANENO YA BABU WA LOLIONDO MGONJWA HAPONI.
MANENO YANAYOTAMKWA ILI DAWA HIYO IINGIE KWENYE KIKOMBE CHA BABU KWA AJILI YA MATIBABU NI SIRI YAKE MWENYEWE NA INAWEZEKANA ATAKUFA BILA WATU WENGINE KUJUA KILE KINACHOTAMKWA ILI MGONJWA APONE.
VIGOGO WANAODAIWA KUTUMIA KINYWAJI CHA BABU VIGOGO MBALIMBALI WANADAIWA KUKIMBILIA KWA BABU AMBI WA LOLIONDO NA KUPATA TIBA YA MARADHI MBALIMBALI YANAYOWASUMBUA.
BAADHI YA VIGOGO HAO NI MAWAZIRI WA JK,JOHN POMBE MAGUFULI NA MILTON MAKONGORO MAHANGA.
WENGINE NI MKURUGENZI WA TAKUKURU,EDWARD HOSEA,IGP MSTAAFU,OMAR MAHITA, RPC WA ZAMANI WA MKOA WA MWANZA,JAMAL RWAMBOW NA MKUU WA MKOA WA MARA,ENOS MFURU.
MARA KWA MARA, MFURU AMEKUWA AKIWATAKA WATU WAAMINI DAWA YA BABU WA LOLIONDO KWA SABABU INATISHA NA YEYE BINAFSI IMEMTIBU.
ASKOFU WA KKKT,THOMAS LAIZER ALIKUWA WA KWANZA KUTOA USHUHUDA KWAMBA DAWA YA BABU AMBI NI NOMA KWA SABABU INA MAAJABU MENGI.
MBUNGE ALIYESABABISHA MGOGORO WA ARUSHA,MARY CHATANDA NAYE ANADAIWA KUTUMIA DAWA YA BABU WA LOLIONDO, KWA HIYO HIVI SASA MAMBO YAKE NI SHWARI.
chanzo cha habari na ibrahim privatus

No comments:

Post a Comment