JINA la muongozaji mahiri wa filamu za Kibongo anayekuja juu hivi sasa, Mshindo Jumanne limezidi kuwa gumzo kutokana na umahiri anaouonyesha kwenye kazi zake anazozifyatua kupitia Kampuni yake ya SSG Distributors.
Baadhi ya mashabiki, wapenzi na wadau wa tasnia ya filamu waliozungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti, walisema kuwa Jumanne ameingia katika orodha ya waongozaji mahiri wa filamu hapa nchini.
Walisema kuwa ameingia kwenye orodha hiyo kutokana na ubora wa kazi zake nyingi, kama vile ‘Honey Moon’, ‘Zuadiswa’ na ‘Cry for Mama’ zilizotokea kukubalika vilivyo kwa watazamaji.
Aidha, kwa upande wake, Jumanne mwenyewe alisema kuwa, hadi sasa ameshafuatwa na kampuni kadhaa kubwa za usambazaji hapa nchini, kuombwa kusaini mkataba wa muda mrefu wa kusambaziwa kazi zake.
Hata hivyo, alisema kuwa anayafanyia kazi maombi ya kampuni hizo kabla ya kuamua kuingia mkataba na mojawapo ama la, ili kuepuka kukurupuka na baadaye kujikuta katika majuto makubwa.
“Unajua nimetoka mbali mno hadi kufikia hapa nilipofika, sasa kama mwanadamu wa kawaida mwenye akili timamu, napaswa kufikiria kwa makini kabla sijajifunga kwa hiyo mikataba,” alisema Jumanne.
Kadhalika, alisema kuwa kampuni atakayokubaliana nayo kuingia mkataba, italazimika kumpa uhuru wa kuendelea kuendesha Kampuni yake ya SSG Distributors huku akiwa ndani ya mkataba huo.
Alisema sababu ya kupigania kuendelea na shughuli za kampuni yake akiwa ndani ya mkataba ni kwa ajili ya kutetea maslahi ya wasanii wake aliowaajiri.MSHINDO JUMANNE ambaye utumia wasanii wachanga yaani underground katika kazi zake amesema baada yakutoa kazi hiyo ya SPECIAL FOR wadau wakae mkao wa kula kwani kuna kazi kibao zinakuja

No comments:
Post a Comment