Wednesday, September 21, 2011

MSHITUKO MKUBWA MWANAUME ALIYETUMIA ARV AOTA MATITI

BAADHI ya wanaume wenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU) wanaotumia dawa za kurefusha maisha wamejikuta wakivimba matiti yao na kuwa makubwa kama ya wanawake. 

Vilevile, wanawake wanaotumia dawa hizo wanalalamika kukutwa na matatizo kadhaa ikiwa ni pamoja na ulemavu.

Joseph Mkanda (43) amekumbana na tatizo la dawa hizo ikiwa ni pamoja na kuvimba matiti.  Mwanzoni alihisi ni kutopata chakula bora, lakini akagundua kwamba ni aina za dawa anazotumia.AKIZUNGUMZA NA PAPARAZI WETU ABDUL CHENJELE ALIYEPIGA KAMBI MTWARA ALISEMA

“Naona aibu sana kutoka nje ya nyumba yangu, kwani nimepata matiti kama mwanamke….  Naona watu wakiniona watanicheka,” anasema mwananchi huyo ambaye ni mkazi wa Mkoa wa Mtwara.

“Nilipokwenda zahanati ya kijijini nikaambiwa hilo ni jambo la kawaida kwa watu walioathirika na Ukimwi, hivyo sijui la kufanya wala pa kwenda,” anasema Mkanda.

Mwanamke Salima Omar (36) mwenye watoto saba  kutoka Mtwara anasema mwili wake umekumbwa na matatizo kibao tangu aanze kutumia dawa hizo.  Mmoja wa watoto wake wa kike alifariki mwaka 2006 muda mfupi tu baada ya kuzaliwa kwake.

Hata hivyo, Salima ambaye ni mke wa Hassan, na ambaye mwili wake umejaa vipele, na maumivu sehemu mbalimbali za mwili, anaamini hali hiyo inatokana na kutopata lishe bora.

“Madawa haya ni makali mno, usipokula vizuri ni lazima yataivuruga afya yako,” anasema na kuongeza kwamba kuna siku analazimika kuyatumia madawa hayo bila kula chochote hususan anapokuwa mgonjwa sana.

Mwanamke huyo anasema kuna wakati hayatumii madawa hayo kutokana na ukosefu wa fedha ya chakula, kwani mumewe ni fundi wa baiskeli na yeye (Salima) hupoteza fedha anazopata kwa kunywea pombe.  Hali hiyo  imemsababishia kuuza mbuzi wote wa familia yake ili kumudu maisha.

Kama zilivyo familia nyingi katika Wilaya ya Mtwara ambazo zinakabiliwa na upungufu wa chakula tangu mwaka 2007, Salima naye yuko katika mkumbo huo.

Vilevile, licha ya kuwa mwathirika, mwanamke huyo bado anaendelea kuzaa.  Miezi mitatu iliyopita alizaa mapacha ambapo mmoja wao alifariki na mwingine hali yake ni mbaya.

Hata hivyo, wataalam wa tiba wamewashauri wanandoa hao kuacha kuzaa, jambo ambalo huenda wakakubaliana nalo.

HAIJAWAHI KUTOKEA NI KICHEN PARTY YA MISS TANZANIA,WATU WASHAANGAA KWANINI IMEKUWA IVI NA NANI HLAUMIWE


Sherehe ya kufundwa (kicheni pati) ya Miss Tanzania namba tatu 2003/04, Nargis Mohamed, imezua gumzo kuanzia maandalizi hadi siku ya tukio mwishoni mwa wiki iliyopita BLOG HII inafunguka.Kwa mujibu wa kinasa habari chetu, tukio hilo la aina yake lilichukua nafasi Jumapili ya Septemba 18, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Karimjee, Posta jijini Dar es Salaam.

Katika shughuli hiyo iliyokuwa na maandalizi ya kihistoria, mastaa kibao wa kike waliohudhuria walijiachia kwa raha zao kutokana na wingi wa mazagazaga kama misosi na vinywaji.

Nyeti zilipenyezwa kwenye gazeti hili kuwa, Nargis ambaye ni Miss Ilala mwaka 2003/04 alifanya kicheni pati hiyo ikiwa ni kukamilisha taratibu za kufunga pingu za maisha Jumamosi ijayo.

Upekupeku wa ‘vuvuzela’ wetu ulibaini kwamba Nargis atafunga ndoa hiyo na mchumba’ke wa siku nyingi aliyetajwa kwa jina moja la Idd ambaye ni mfanyakazi wa benki moja jijini Dar.

Sherehe za harusi ya Nargis zinatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa The Star Rune Mikocheni, Dar.

KILA LA KHERI NARGICY KATIKA NDOA YAKO

MSHITUKO JIJINI,MAREHEMU TABIA WA KIDEDEA AFUFUKA WATU WACHANGANYIKIWA













Pamoja na kutangulia mbele za haki mwanzoni mwa mwaka huu, Watanzania watapata fursa ya kuona vimbwanga vya aliyekuwa mwigizaji mkubwa Bongo, marehemu Dalillah Peter Kisinda ‘Tabia’ katika muvi yake ya mwisho ya Naomi inayokimbiza sokoni.

Kwa mujibu wa mtayarishaji wa filamu hiyo, Hamis Kibari, watakaoitazama muvi hiyo watagundua kwamba Tabia aliyevuma na Kundi la Kidedea alikuwa hazina kubwa ya uigizaji Bongo kwa jinsi alivyomudu vizuri nafasi yake.

“Tabia alifariki dunia wakati tunajipanga kutengeneza ‘part II’ ya filamu hii… Lilikuwa ni pigo kubwa kwetu lakini tumeamua kuwaonesha Watanzania kazi yake ya mwisho kabisa duniani hivyo ni kama ‘amefufuliwa’ upya,” alisema Kibari na kuongeza:

“Mbali na Tabia, Filamu ya Naomi imewashirikisha mastaa wengine kama Bakari Makuka (Beka), Leah Mussa (Shaster) na Suzane Lewis (Natasha).”
Khamisi Kibari ambaye ndiye muundaaji wa filamu hiyo amessema filamu hiyo ipo sokoni na inagombaniwa kama maji