Thursday, June 30, 2011

JACKLINE WOLPER ABANWA

Hemed Kisanda na Jelard LucasMastaa ‘kapo’, Jacqueline Wolper na Nassib Abdul ‘Diamond’ ambao uhusiano wao kimapenzi umekuwa ukitengeneza vichwa vya habari, wanaendelea kujikanganya, ishu kamili ipo aya zinazofuata.The First Class Paper, Ijumaa lilimnasa Jacqueline Jumatatu ya wiki hii, saa 4 usiku na kumbana kwa maswali mfululizo kuhusu Diamond kutokana na ukweli kwamba, yeye ndiye yupo mstari wa mbele kukanusha ukweli.Akiwa amekolea ‘make up’ tayari kurekodi muvi mpya inayoitwa Mafisadi, Kijitonyama Sayansi, Dar, Jacqueline alisema kwa kujikanyaga kwamba anamfahamu Diamond kama msanii mwenzake na wanashirikiana tu kikazi.“Namfahamu kama mwanamuziki na sijawahi kumjua kwa jambo lingine zaidi,” alisema Jacqueline.Alipouliza ushirikiano gani walionao, yeye akiwa staa wa filamu na Diamond ni mwanamuziki, staa huyo ambaye pia anatambulika kama pacha wa Ijumaa Sexiest Girl 2008-09, Irene Uwoya, alijibu:“Diamond ana filamu yake anayotaka kuitoa na amesema atashirikiana na mimi. Amesema mimi nafaa kushiriki muvi yake, kwahiyo tunashirikiana kwa staili hiyo.”Hata hivyo, akionesha kuwa amejipanga kukwepa kila swali, Jacqueline alitoa macho kwa mshangao, pale paparazi wetu alipomueleza kwamba zipo ‘data’ zinazomthibitisha alipomkoromea Diamond kwa kuvujisha siri ya uhusiano wao.Jacqueline akiwa haamini alichokisikia, alisema: “Mmh, nanyi mnafuatilia vitu!”Mrembo huyo alikosa swali alipotajiwa jina la hoteli moja iliyopo Magomeni Kagera, Dar ambayo ndiyo hukutana na Diamond kwa ajili ya mambo yao.Kijasho kilimtoka Jacqueline, alipoambiwa kuwa alimpigia simu Diamond na kumlaumu kwamba hana siri, siku ambayo uhusiano wao wa kimapenzi ulipoandikwa kwa mara ya kwanza na gazeti la Risasi.Badala ya kupangua hoja, Jacqueline alisema: “Nyinyi watu wa Global Publishers (wachapishaji wa Ijumaa) ni hatari sana, yaani hata hilo mnajua?”Alipozungumza hivyo, Jacqueline alinyanyuka na kuondoka kwa maelezo kwamba muongozaji wake alikuwa akimhitaji kwa ajili kwa ajili ya kuanza kurekodi filamu.Baada ya kuachana naye, siku iliyofuata, paparazi wetu ‘alimbananisha’ tena Jacqueline Bamaga Mwenge, Dar na kuendeleza maswali juu ya uhusiano wake na Diamond ambapo alijibu:“Ndani ya nafsi yangu najua Diamond ananipenda sana lakini mimi siwezi kutoa penzi langu kwake kwa sababu naogopa umri wake mdogo atadata.”Pamoja na majibu hayo, Ijumaa lina vielelezo kuwa Jacqueline na Diamond wanaitana majina ya sweet na honey lakini wao wenyewe hawataki watu wajue.endelea kusoma blog yangu ili kujua nini kitaendelea









IRENE UWAYO MAMBO SAFI

    "JAMANI TUMEPENDEZA NA WENYE WIVU MTAJIJU":Irene akiwa amembeba mwanawe.  Pembeni ni mumuwe Ndikumana.
Akiwa na mwanaye.
    "MAMA IRENE IVI KWELI HUYU MTOTO NI WA HUYU JAMAA AU NDO KASINGIZIWA MBONA KAFANANA NA H.MAMA NA KALE KAMGUU KAMA CHA KASUMBA THE GREAT NA KASURA MMH NI KAMA CHA YULE BUHESHIMIWA WA MJENGONI KULE AU WEWE UNAONAJE MAMA" Mama mzazi wa Irene (kushoto) na baba yake (kulia) wakiwa katika hafla hiyo.
          MZEE CHILO: "MTOTO KAFANANA NA KASUMBA THE GREAT HUYU BANA" Msanii wa filamu  Mzee Chillo (kulia) akiwa na  Ndikumana na Irene na msanii wa filamu ambaye jina lake halikufahamika mara moja wakati wa sherehe ya kumtoa mtoto Krish iliyofanyika juzi Jumamosi huko Mbezi Jogoo, jijini Dar es Salaam.
      KAMBI:JAZA KABISA KWENYE KULA HAKUNA UMAHARUFU MAMA"Hasheem Kambi (kulia) akiwa katika msafara wa kupata chakula.
      "JAMANI MIMI SIJUI KISWAHILI VIZURI NYIE ENDELEENI TU KUPIGA DUA"Msanii wa filamu Hasheem Kambi (katikati) akiwa na Ndikumana (kushoto)  na Mzee Chillo.
     "MALIZA HARAKA HIYO DUA BANA UBWABWA UNAPOA KULE"Mzee Chillo na msanii mwenzake wakimswalia Krish. SHEREHE ya kumtoa mtoto Krish wa mcheza filamu maarufu nchini, Irene Uwoya, iliyofanyika Jumamosi nyumbani kwao Mbezi Jogoo, jijini Dar es Salaam, imefana baada ya kuhudhuriwa na watu kibao ambao walisherehekea siku hiyo kwa kila aina ya burudani.
Miongoni mwa waliohudhuria ni wasanii mbalimbali wa filamu na muziki

Tuesday, June 28, 2011

LULU:NIKIVAA NGUO NDEFU NAWASHWA

MSANII anayezidi kungara kwenye filamu mbalimbali Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, amedai kuwa, anapenda kuvaa nguo fupi kwa sababu akivaa nguo ndefu anawashwa. Akizungumza na mwandishi wa habari hii juzi ndani ya Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, Dar es Salaam, Lulu alisema kuwa, hiyo ndiyo sababu kubwa ambayo inamfanya kila anapotoka avae nguo hizo za kihasarahasara.
“Yaani  huwezi kuamini, nikivaa nguo ndefu, basi siku hiyo nitajikuna sana maana nitawashwa mwili mzima, kuanzia kiunoni, hasa mapajani kuelekea miguuni,” alisema msanii huyo na kuongeza:
“Ujue kuvaa kwangu nguo fupi siyo kwamba naiga kwa watu wengine, tangu nikiwa mtoto nilikuwa navaa hivyo na ndiyo maana kubadilika ni ngumu kidogo.”
Lulu ni msanii wa kike mwenye umri mdogo ambaye mara kadhaa amekuwa akilalamikiwa kutokana na tabia yake ya kuvaa nguo fupi wakati anapoto mitoko lakini Luli mwenyewe amesema haoni sababu ya waandishi wa habri wa magazeti kumfatilia kwa sababu yeye mwenyewe ndivyo anavyopenda kwa hiyo amesema wafanye mambo mengine na sio kumfatilie maisha yake

 "EEEEEH NGOJA NICHEKE MIE" NDIVYO ANAVYOONEKA AKISEMA HAPO AKIWA KATIKA VAZI LA ................ AMBALO BAADHI YA WATU WAKIONA BASI BOXER LAZIMA ZIACHIE MADOWA
 "EBU NIWEKE POZI ILI KWA RAHA ZANGU"LULU AKIWA KATIKA MOJA YA PICHA AMBAZO ANAONEKANA AKIWA AMEVAA NGUO FUPI
 "ONGEENI SASA NIPO KIAFRIKA ZAIDI"DUH HII SASA NI HATARI LULU

"NA BADO MTASEMA SANA"

Thursday, June 23, 2011

MSHINDO JUMANNE AZIDI KUKAMATA SOKO LA FILAMU

JINA la muongozaji mahiri wa filamu za Kibongo anayekuja juu hivi sasa, Mshindo Jumanne limezidi kuwa gumzo kutokana na umahiri anaouonyesha kwenye kazi zake anazozifyatua kupitia Kampuni yake ya SSG Distributors.
Baadhi ya mashabiki, wapenzi na wadau wa tasnia ya filamu waliozungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti, walisema kuwa Jumanne ameingia katika orodha ya waongozaji mahiri wa filamu hapa nchini.
Walisema kuwa ameingia kwenye orodha hiyo kutokana na ubora wa kazi zake nyingi, kama vile ‘Honey Moon’, ‘Zuadiswa’ na ‘Cry for Mama’ zilizotokea kukubalika vilivyo kwa watazamaji.
Aidha, kwa upande wake, Jumanne mwenyewe alisema kuwa, hadi sasa ameshafuatwa na kampuni kadhaa kubwa za usambazaji hapa nchini, kuombwa kusaini mkataba wa muda mrefu wa kusambaziwa kazi zake.
Hata hivyo, alisema kuwa anayafanyia kazi maombi ya kampuni hizo kabla ya kuamua kuingia mkataba na mojawapo ama la, ili kuepuka kukurupuka na baadaye kujikuta katika majuto makubwa.
“Unajua nimetoka mbali mno hadi kufikia hapa nilipofika, sasa kama mwanadamu wa kawaida mwenye akili timamu, napaswa kufikiria kwa makini kabla sijajifunga kwa hiyo mikataba,” alisema Jumanne.
Kadhalika, alisema kuwa kampuni atakayokubaliana nayo kuingia mkataba, italazimika kumpa uhuru wa kuendelea kuendesha Kampuni yake ya SSG Distributors huku akiwa ndani ya mkataba huo.
Alisema sababu ya kupigania kuendelea na shughuli za kampuni yake akiwa ndani ya mkataba ni kwa ajili ya kutetea maslahi ya wasanii wake aliowaajiri.MSHINDO JUMANNE ambaye utumia wasanii wachanga yaani underground katika kazi zake amesema baada yakutoa kazi hiyo ya SPECIAL FOR wadau wakae mkao wa kula kwani kuna kazi kibao zinakuja

HUU NI UDHALILISHAJI WA KIJINSIA

MOJA YA SCENE AMBAZO ZIPO KWENYE FILAMU IVI AMBAYO NISINGEPENDA KUITAJA IKIONYESHA JINSI GANI WASANII WACHANGA WANAVYOZALILISHWA BINTI HUYU ALIAMBIWA AVUE NGUO ETI KWAKUWA SEHEMU YA IKO CHUMBA AMBACHO WANATAKA KUSGOOT KUNA JOTO SANA KWA HIYO ALIAMBIWA AVUE NGUE ILI WAWEZE KUSHOOT VIZURI BILA KUHARIBU CAMERA IVI NI KWELI?

LIMEJAA VIPAJI VIPYA

MFANO WA GARI AMBALO MSHINDO JUMANNE ANASEMA NI MFANO WA ROLI LILILOJAA VIPAJI AMBAVYO MUDA SI MREFU VITAANZA KUONEKANA KUPITIA KAZI MBALIMBALI ANAZOTARAJIA KUZITOA

NIMEKUJA KUWASHIKA

 KWA JINA ANAJULIKANA KAMA MSHINDO JUMANNE MSANII MKONGWE WA FILAMU MWENYE VIPAJI LUKUKI KAMA VILE KUANDAA NA KUONGOZA FILAMU (DIRECTER) ANAYEKUJA UPYA KWA LENGO LA KUONDOA UKIRITIMBA KATIKA TASINIA HII YA FILAMU NCHINI KWA LENGO LA KUWATUMIA WASANII CHIPUKIZI KATIKA KAZI ZAKE NA KUACHA KUTUMIA MAJINA MAKUBWA AMBAYO TEYARI YAPO KATIKA MASIKIO YA WATU."LENGO LA KUU NI KUONDOA UKILITIMBA KATIKA TASINIA HII YA FILAMU NCHINI AMBAYO INAONEKANA KUWA NA USHABIKI KULIKO VIPAJI VYA WASANII,UKIANGALIA SASA IVI WATU HAWAANGALII KAZI YA MTU BALI NI JINA LA MTU WANAANGALIA NANI KAIGIZA KATIKA HIYO FILAMU NA SI NINI KIMEFANYIKA KATIKA HIYO FILAMU". HAYA NI MANENO YAKE GWIJI ILO LA FILAMU NCHINI KWA SASA MSANII HYO AMETOA FILAMU INAYOKWENDA KWA JINA LA "SPECIAL FOR YOU" AMBAYO TEYARI IPO MADUKANI.
KWA JINA ANAITWA IBRAHIM PRIVATUS NI KIJANA MWENYE KIPAJI CHA KUIGIZA NA UTUNZI WA FILAMU AMBAYE MSHINDO JUMANNE AMEKIONA KIPAJI HIKI NA KUSEMA UNAFAHA KATIKA KAZI ZANGU KWA SASA WAPO KATIKA MIPANGO MBALIMBALI IKIWEMO KUTENGENEZA FILAMU AMBAYO ITAFUNIKA KABISA SOKO LA FILAMU NCHINI NA NJE YA NCHI JINA LA FILAMU HIYO LIMEHIFADHIWA KWA SASA,MSHINDO JUMANNE AMEWAAMBIA WADAU WA FILAMU NCHINI WATARAJIE MENGI KUTOKA KWA IBRAHIM PRIVATUS.

Monday, June 20, 2011

WASEMAVYO MASTAA WA FILAMU NCHINI

 BLACK HAND FILAMU INAYOTIKASA KATIKA SOKO LA FILAMU NCHINI.PATA NAKALA YAKO SASA ILI UONE NINI KIMEJILI NDANI YA BLACK HAND
 ROSE NDAUKA MSANII WA KIKE ANEYEJUA DHAMANI YAKE YA UIGIZAJI

 WASTARA:KIPAJI TOKA MOYONI
 AUNT EZEKIEL:MAGAZETI HAYANIZIBI MDOMO WANGU

 DUH ILO POZI MMH MIMI YANGU MACHO

THEA:NAFANYA NINACHOJISIKIA JAMANI

Thursday, June 16, 2011

FILAMU YA SPECIAL FOR YOU SASA MITAANI KUPITIA KWA SSG


Kampuni ya SSG DISTRIBUTORS kusambaza filamu ya Special for you nchi nzima akiongelea filamu hiyo Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya SSG iliyopewa dhamana ya kusambaza filamu hiyo alisema filamu hiyo itaingia sokoni Jumatatu tarehe 20Th June 2011. Miezi kadhaa iliyopita Mshindo alinukuliwa akisema sasa kampuni yake haitosambaza tena filamu na badala yake itakuwa ikitayarisha tu na jukumu la kusambaza litakuwa chini ya kampuni ya Steps Entertainment.

Mwandishi wa habari hizi alipotaka kujua sababu za SSG kusambaza wenyewe filamu hii alisema wamelazimika kufanya hivi ili kukata kiu ya washabiki wao ambao walikuwa wakisumbua kupiga simu mara kwa mara kuhoji ni kwanini hawaoni filamu mpya iliyoandaliwa na SSG. Mshindo aliendelea kusema kutokana na ratiba ya Steps inaonyesha filamu zilizotayarishwa na SSG zitaanza kutoka kati ya September na October
.
Mshindo Jumanne Latifa Idabu
Mshindo Jumanne Latifa Idabu wakibusiana.
“Ratiba inaonyesha kuwa filamu zangu zitasambazwa miezi hiyo niliyosema hivyo nimeona ni mbali sana kwa washabiki wangu kuendelea kusubiri mpaka muda huo ndipo nikaonana na Uongozi wa Kampuni ya Steps unipe ruhusa nisambaze mwenyewe filamu yangu angalau moja na nashukuru wamenielewa na wamenipa support kubwa katika kufanikisha zoezi hilo” Anasema Mshindo. Filamu ya Special for you itakuwa ni filamu ya kwanza iliyoandaliwa na Mshindo kutoka mwaka huu baada ya Ushuhuda wa Mariam iliyotoka mwishoni mwa mwaka jana na ijapokuwa mwanzoni mwa mwaka huu ilivuma SSG ingetoka na filamu ya MTANDAO lakini filamu hiyo ndiyo ilikuwa ya kwanza kudakwa na Kampuni ya STEPS Entertainment.
Akizungumzia ujio huo mpya wa filamu ya Special for you Mshindo alisema ni filamu bora kuliko filamu zake zote alizowahi kutoa ambapo picha zake zimepigwa katika maeneo ya Kilombero Morogoro na Dar es salaam.
Baadhi ya washiriki wanaopatikana katika filamu hiyo mpya ni Hashim Kambi, Deogratius Shija, Niva, Zamda Mwera, Bi Zuki, Rashid Yussuph, Mshindo Jumanne mwenyewe na wasanii wengine wengi wanaofanya vizuri kwa sasa.
Mshindo amewataka mawakala wote wa mikoani na Dar es salaam ambao wangependa kuuza Filamu hiyo wawasiliane naye kupitia namba 0658 420400, 0768 686634, 0786 420400 na 0773 410420.